Mix

Hiki ndio ulikuwa unakisikiliza mwaka mzima

on

Boomplay, App namba moja ya kusikiliza na kupakua muziki iliyo chini ya Kampuni ya Transsnet Music Limited imeonyesha matarajio makubwa ya kupaa kwa tasnia ya muziki wa Tanzania katika anga za Kimataifa mwaka 2022.

Hayo ni kwa mujibu wa muhtasari wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo ambayo ina ofisi nchini Tanzania, Nigeria, Ghana, Kenya na hivi karibuni nchini Ivory Coast.

Programu hiyo tumishi inapatikana duniani kote kwenye simu kupitia Google Play Store ya Android, App Store ya iOS na kwenye wavuti kupitia www.boomplay.com.

Kwa sasa Boomplay ina zaidi ya watumiaji milioni 60 kwa mwezi (MAU’s) na zaidi ya nyimbo milioni 65.

2021 umekuwa mwaka mgumu. Hiyo ni kweli. Lakini kuna sababu za kuwa wachangamfu tunapoelekea 2022.

Mwaka 2021 ulikuwa ni mwaka wa kupeperusha bendera ya muziki.

“Nchini Tanzania, tumeona mabadiliko katika tasnia ya muziki kama vile tasnia ya muziki kuingizwa katika sera na sekta rasmi.

“Tumeona aina za muziki mpya wa staili ya Amapiano na Singeli zikihusika sana kuiteka tasnia ya Bongo flava.

“Huu ni mwanzo na kuna safari ndefu, lakini yote kwa yote, 2021 imetupa sababu za kuwa na matumaini makubwa kwa 2022,”imeeleza taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Kampuni hiyo, Boomplay ilitoa muhtasari wake wa kila mwaka Desemba 7, ambao ulionesha namna wasanii kama Rayvanny, Mbosso na Alikiba walishika nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu katika kipengele cha ‘Most Streamed Maleartists’.

Huku wenzao wa kike, Zuchu, Nandy na Anjella, wakifanya vizuri zaidi katika kipengele cha ‘Most Streamed Female artists.

Aidha ni vyema kutambua kuwa, Zuchu ameshika nafasi ya kwanza kwa miaka miwili mfululizo.

Katika mwaka ambao albamu zaidi ya tano na EP zimetolewa kupitia Boomplay, mafanikio makubwa yameonekana kupitia msanii wa Hip-Hop nchini ‘Stamina ambaye albamu yake “Paradiso”, iliyotokamwezi Novemba, ilipata jumla ya streams milioni moja ndani ya wiki moja tu kupitia Boomplay.

Boomplay Recap 2021 inaonesha wasanii na nyimbo ambazo zimetufanya tutikise kichwa mwaka mzima huku tukiangazia nini kilichosikilizwa na mtu mmoja mmoja. Ndani ya App ya Boomplay, sasaBoombuddies wanao uwezo wa kuangalia nini walichokuwa wakisikiliza kulingana na matumizi yao ya kila siku ndani ya mwaka mzima wa 2021 na kuweza kuonesha aina ya muziki na ladha wanazozipenda ambapo wanaweza kutuma kwa marafiki.

Kiambatanisho cha #MyBoomplayRecap2021, ambao ni muhtasari wa watumiaji wa Boomplay unaangazia safari ya muziki ya watumiaji kwenye Boomplay, ikieleza kwa kina idadi ya nyimbo walizosikiliza katika mwaka huu, aina ya muziki wanaoupenda, wasanii wanaowapenda na ladha nyingine.

Mwezi Oktoba, Boomplay ilitia saini ya ushirikiano mkubwa na Billboard, ambapo takwimu za kusikiliza muziki katika App ya Boomplay ziliongezwa kwa takwimu za chati hizo maarufu duniani.

Maendeleo haya yanafungua fursa nyingi kwa wasanii wengi wa Kiafrika kupata fursa saw ana wale wa kimataifa kupitia jukwaa la kimataifa la ‘Billboard’ huku pia ikionyesha talanta (vipaji) vikubwa katika bara zima.

Soma na hizi

Tupia Comments