Mali za Mastaa

Kipaji kinalipa… hapa kuna picha ya Mbwana Samatta na gari lake jipya.

on

IMG_4680.JPGSamatta anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji watanzania wanaoingiza fedha nyingi kupitia soka – akiripotiwa kulipwa mshahara usiopungua $8000 kwa mwezi bila kuongeza marupurupu.

Mmoja ya wachezaji wa kitanzania wenye mafanikio katika soka nje ya mipaka ya Tanzania, Mbwana Samatta leo asubuhi ameposti picha ya gari lake jipya analotumia akiwa nchini Tanzania.

Gari aliloposti Samatta ni Range Rover lenye rangi ya damu ya mzee ambalo lina namba za usajili za Tanzania na linakua gari la pili la thamani ambalo Samatta ameliweka hadharani baada ya mwaka 2013 kulionyesha gari lake aina ya Chrysler Crossfire ambalo lilikuwa na thamani ya takribani millioni 50 za kitanzania.  Samatta alijiunga na TP Mazembe akitokea Simba SC kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi kwa kipindi hicho ya $100,000.

Kuna kitu gani Samatta amewahi kufanya uwanjani huwezi kukisahau?

Soma na hizi

Tupia Comments