Mix

T.I alisema hawezi kumchagua mwanamke kuwa Rais wa Marekani, Kanye West na Jay Z je?

on

Baada ya kutangaza nia yake ya kugombea Urais wa Marekani kufikia mwaka 2020, Kanye West amekuwa akiweka headlines nyingi zinazohusiana na viongozi wa Siasa.

CLINTON7

Mgombea Urais wa Marekani kwa mwaka 2016, Mama Hillary Clinton.

Licha ya rapper T.I kuonyesha wazi kuwa hatotoa kura yake ya Urais kwa mwanamke, Hillary Clinton ambaye pia ni mgombea Urais, Kanye West ameonekana kuwa na nia tofauti kabisa… kwa mujibu wa mtandao wa Buzzfeed, rapper na producer Kanye West ameamua kuweka nguvu zake kwa mgombea huyo na kuamua kuchangia pesa za kuendesha kampeni za mgombea Urais, Hillary Clinton anaegombea Urais kupitia Chama cha Democratic Party, alichopo Rais Barrack Obama.

CLINTON

Kanye West & Hillary Clinton.

Japo mtandao wa Buzzfeed, haujaweka wazi ni kiasi gani cha pesa ambacho Kanye West kaamua kutoa kwenye kamati ya Mama Hillary, Kanye sio msanii wa kwanza wa HipHop kutoa support hiyo kwa mama huyo… rapper Ja Rule pia hivi karibuni alisikika akisema kuwa support yake kubwa ameiweka kwa mgombea huyo zaidi.

SAN JOSE, CA - OCTOBER 15: Ja Rule attends the "I'm In Love With A Church Girl" premiere at California Theatre on October 15, 2013 in San Jose, California. (Photo by Trisha Leeper/WireImage)

Ja Rule.

Jay Z pia ameonekana akishirikiana na kamati ya kampeni ya Hillary Clinton kwa ukaribu sana, huku kamati hiyo ilitumia zaidi ya dola 15, 000 ambayo ni sawa na milion 34 za Kitanzania kwenye restaurant ya Jay Z ’40/40′ kwa ajili ya catering, chakula na vinywaji mwezi uliopita.

CLINTON3

Jay Z & Kanye West.

Wasanii wengine wanaomuunga mkono Mama Hillary Clinton ni Jessica Alba, Matt Damon na Tom Hanks ambao wote pia tunaambiwa wamechangia kwa namna moja ama nyingine kugharamia kampeni za Mama Hillary Clinton.

CLINTON6

Jessica Alba.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments