Kiungo Mtanzania Himid Mao Mkami anayecheza club ya Ghazl El Mahallah ya Misri jana wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Misri dhidi ya Future SC uliyomalizika kwa sare ya 0-0.
Himid alianguka baada ya kugongwa kichwani na mchezaji wa Future wakati wakiwania mpira tukio ambalo lilishtua watu wengi ikiwemo wachezaji wa pande zote na kupelekea mchezo kusimama.
Baada ya mchezo muda mfupi uliopita Himid Mao amethibitisha kupitia AyoTV kuwa hajaumia sana na vipimo vya awali vimeonesha yuko sawa hivyo hawezi kusema kama atakuwa nje ya uwanja au la ila kwa sasa ameonekana yuko sawa.