Habari za Mastaa

Wasanii wenye misamiati mingi zaidi kwenye Hip Hop Marekani ni…? Wajue hapa.

on

Image copyright Adrian Platts and DetroitBikeBlog http://adrianplatts.com

Nimekutana na stori kwenye moja ya mitandao inayoonyesha wanamuziki wa hip hop Marekani Eminem, Kanye West na Jay Z wanafanana kitu kimoja…utumiaji mwingi wa misamiati mikubwa kwenye nyimbo zao.

eminem2

Eminem

Kutokana na utafiti mpya uliofanyika, wasanii hawa wa tatu ni miongoni mwa wasanii tano bora wenye misamiati mingi zaidi kwenye industry ya muziki Marekani. >>>“Nia ni kulinganisha ukubwa wa utumiaji wa misamiati wa hawa wananuziki”<<< hii ni nukuu ya moja ya sentensi kutoka kwenye utafiti huo .

jay z2

Jay Z

Kuna baadhi yao wamefanikiwa kuwa na idadi kubwa ya mashabiki mpaka leo kwasababu ya sanaa yao na jinsi ambavyo wameweza kutumia  misamiati kuwagusa mashabiki…Utafiti huo umetumia orodha ya wasanii 99 bora duniani, wamelinganishwa na kuchujwa kwa kuhesabu idadi ya misamiati ya kipekee waliotumia kwenye nyimbo zao zote.

PageSix Cannes, FRANCE. 17th June- Steve Stoute, founder CEO of Translation, Ben Horowitz, Co-founder, Partner Andreessen Horowitz and American rapper, songwriter, record producer, film director, entrepreneur, and fashion designer Kanye Omari West. Pic. Ella Pellegrini

Kanye West 

Eminem aliibuka kidedea akiwa na idadi ya misamiati 8,818 ya kipekee kwenye nyimbo zake akifuatiwa na rappa Jay Z akiwa na idadi ya misamiati 6, 899 , Marehemu Tupac Shakur akiwa na idadi ya misamiati 6,569 na Kanye West akiwa na idadi ya misamiati 5,069.

tupac

2 Pac

Mtunzi wa nyimo Bob Dylan ameshika nafasi ya tano akiwa na idadi ya misamiati 4,883 na ni msanii pekee asiyefanya muziki wa hip hop kushika nafasi hiyo. Kitendo cha wasanii wa Hip Hop kushika nafasi zote 4 za juu pengine sio kitu cha kushangaza sana kwani wengi tunafahamu kuwa asili ya muziki wa Hip Hop umejengwa kwenye misingi ya kutumia mistari yenye misamiati migumu.

bob dylan

Bob Dylan

Wewe unauonaje uchambuzi huu mtu wangu? unakubaliana na hii orodha ama unahisi ni msanii gani wa Hip Hop Marekani anatakiwa pia kuwepo kwenye hii 5 bora?

 PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments