Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Hizi ndio rekodi na sifa za kocha mpya wa Manchester United

on

960150_10152470478372853_7242101775726307286_nHatimaye Manchester United wamemtangaza rasmi Louis Van Gaal kuwa kocha wao kuanzia msimu ujao.

Louis Van Gaal ambaye alizaliwa miaka 62 iliyopita nchini Uholanzi anakuwa kocha wa kwanza kabisa kutoka nje ya Uingereza na visiwa vyake kuifundisha klabu ya Manchester United.

Van Gaal amewahi kuvichezea vilabu vya Ajax, Royal Antwerp, Telstar, Sparta Rotterdam, AZ Alkmaar, pia amewahi kuvifundisha vilabu vya Ajax ambapo alishinda vikombe vitatu vya ligi kuu, vikombe vitatu vya michuano ya Johanny Cruyff, kombe moja la Champions League, UEFA Cup mara 1, na kombe la mabara vilabu mara 1.

Akatoka Ajax na kuhamia FC Barcelona ambapo alichangia sana kuwainua makinda akina Lionel Messi, Xavi Hernandez na Andres Iniesta pamoja na kipa Victor Valdes – aliwawezesha kushinda La Liga mara 2, UEFA SuperCup 1, Copa 1.

REKODI NYINGINE KAMA UNAVYOWEZA KUONA KWENYE PICHA.

1907627_10152470343587853_9142793400015469852_nKama unataka stori kama hizi zisikupite ungana na mimi kwenye twitter kwa kubonyeza HAPA, pia FACEBOOK & INSTA ili niwe nakutumia kila stori inayonifikia.

Tupia Comments