Michezo

Hizi ndizo Timu mbili kubwa za Ligi Kuu ya Uingereza zinamtaka Samatta

on

Mtanzania Mbwana Samatta baada ya kuandika record ya kuwa mtanzania wa kwanza kucheza na kufunga goli katika uwanja wa Anfield kwenye game ya UEFA Champions League hatua ya Makundi kati ya timu yake ya Genk dhidi ya Liverpool.

Amerudi tena kwenye headlines za usajili, Samatta Jumanne ya wiki hii alikuwa sehemu ya kikosi cha Genk kilichocheza dhidi ya Liverpool, Genk wakapoteza kwa kufungwa 2-1 lakini Samatta alifunga goli dakika ya 41.

Baada ya kufunga goli hilo ambalo ni goli lake la pili UEFA Champions League msimu huu, mtangazaji wa mechi za mpira wa miguu wa kituo cha BBC Sports Ian Dennis ameandika kuwa Samatta ameanza kuhitajika na klabu za West Ham United na Newcastle za England.

Hivyo Genk wakiwa wanasubiri kumalizia game zake mbili za kukamilisha ratiba za UEFA Champions League huenda tukamuona akitua England Janury katika dirisha dogo la usajili.

ZAHERA AFUNGUKA “NIMETOA ZAIDI YA MILIONI 100 YANGA, SITOWADAI, WACHEZAJI PIA WAMENIKOPA”

Soma na hizi

Tupia Comments