Staa wa Tanzania aliyejiunga na Club ya CD Tenerife ya Hispania August 2018 akitokea Azam FC, Shaban Iddi Chilunda ameripotiwa kutolewa kwa mkopo na club yake hiyo na kwenda katika club ya CD Izarra ya Hispania pia.
Chilunda mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na CD Tenerife August 2018 kwa mkataba wa miaka miwli na sasa ametolewa kwa mkopo wa miezi sita kwenda club ya CD Izarra, hivyo Tenerife wamempeleka huko ili apatae nafasi ya kucheza zaidi.
Staa huyo ni zao la Academy ya Azam FC na sasa anaenda kucheza CD Izarra inayoshiriki Ligi daraja la pili nchini Hispania (Segunda Division B) akitokea club ya CD Tenerife inayoshiriki Ligi daraja la kwanza Hispania maarufu kama (Segunda Division).
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”