Michezo

Pigo walilopata FC Bayern kabla ya kucheza na Real Madrid

on

Club ya FC Bayern Munich ya Ujerumani leo Jumanne ya April 17 2018 imezipokea taarifa mbaya kuhusiana na kiungo wake wa kimataifa wa Chile Arturo Vidal kuwa atakosekana mchezaji huyo kwa mechi zote za msimu za Bayern Munich zilizosalia.

Arturo Vidal atakakosekana katika game zote za FC Bayern zilizosalia baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti na kugundulika kuwa jeraha hilo haliwezi kupona mapema, Vidal ameifungia Bayern magoli 6 katika game zake 22 za Bundesliga alizozichezea msimu huu.

Game yake ya mwisho Vidal kuichezea Bayern ilikuwa ni game dhidi ya RB Leipzig iliyomalizika kwa Bayern kupoteza kwa magoli 2-1 wakiwa nyumbani, kwa maana hiyo ni wazi Vidal atakosekana katika michezo miwili muhimu ya nusu fainali ya UEFA Champions League kati ya FC Bayern Munich dhidi ya Real Madrid.

Kabla ya hapo Vidal alionekana uwanjani akiitumikia FC Bayern kwenye mchezo wa robo fainali wa kwanza dhidi ya Sevilla lakini alitolewa dakika ya 36 baada ya kushindwa kuendelea na mchezo.

ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1

Soma na hizi

Tupia Comments