Michezo

Man United wameamua kuwa serious walimtoa shabiki uwanjani vs Liverpool

on

Kufuatia kushamiri kwa vitendo vya ubaguzi wa rangi barani Ulaya na baada ya kuoneshwa vitendo hivyo wachezaji wa England wenye ngozi nyeusi wa wakati wa mchezo dhidi ya Bulgaria, club ya Man United yenyewe imeamua kuwa wakali zaidi kutokana na kukemea kwa vitendo.

Imeripotiwa kuwa kuelekea mchezo wao dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Old Trafford uliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1, walimtoa shabiki wao aliyekuwa anatazama mchezo huo kutokana na kujaribu kumuonesha vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa rangi kwa beki wa Liverpool Trent Alexander-Arnold.

Tukio hilo lilitokea wakati wa kipindi cha kwanza ndipo walinzi wa uwanja wa Man United stewards walipoamua kumtoa nje ya shabiki huyo baada ya kudwai kuwa walisikia akisema ‘you f***ing black c**t’ kwa Alexander-Arnold beki wa Liverpool, sasa hivi waingereza baada ya kubaguliwa kwa wachezaji hao wameweka mkazi zaidi kuhakikisha vitendo hivyo vya ubaguzi vinakoma.

AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments