AyoTV

Kama unataka mkopo wa Elimu ya Juu, kuna hii ya kufahamu kutoka RITA

on

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini RITA imewataka Waombaji wa mkopo wa Elimu ya Juu kuhakiki vyeti vya kuzaliwa na vifo kabla ya kuviwasilisha kwa Bodi ya Mikopo na kusisitiza kuwa hakuna mwanafunzi atakayepata mkopo bila ya kuhakiki nyaraka hizo.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Emmy Hudson amewakumbusha waombaji hao kufikisha nyaraka zao Makao Makuu yaOfisi hizo Dar es Salaam, na Wilaya zote za Tanzania Bara kwa ajili ya uhakiki ili kukidhi masharti ya kupata mkopo.

Aidha, ametoa wito kwa waombaji hao kutodanganya taarifa zozote kwenye nyaraka hizo ili waweze kupata mikopo na kwamba kwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwenye video hii kuna kila kitu…play kutazama!.

FAHAMU: Kuhusu mfumuko wa bei na thamani ya Shilingi…je, imeimarika? Jua zaidi kwa kuplay kwenye hii video!!!

Soma na hizi

Tupia Comments