Michezo

Good News: Hasheem Thabeet mbioni kurudi NBA

on

Mtandao wa bleacherreport.com umeripoti kuwa mtanzania Hasheem Thabeet mwenye umri wa miaka 32 yupo mbioni kurudi kucheza Ligi Kuu ya kikapu nchini Marekani (NBA) akihusishwa kujiunga na timu ya kikapu ya New York Knicks.

Taarifa za Hasheem Thabeet kurejea NBA zimeenea kwe baadhi ya vyombo vya habari za michezo jijini New York, kama mazungumzo na New York Knicks wakifanikiwa kumshawishi na kukubaliana nao basi staa huyo atarejea NBA kuendeleza kipaji chake.

Bado kuna na nafasi ya New York Knicks kumsajili Hasheem Thabeet kwani hadi sasa wanawachezaji 19 walio na mikataba, hivyo nafasi iko wazi kwa Hasheem kama wataonesha dhamira ya kweli, Hasheem amecheza NBA katika timu kama za Memphis Grizzlies, Houston Rockets, , Portland Trail Blazers, Oklahoma City Thunder na Grand Rapids Drive kabla ya 2017 kujiunga na Yokohama B-Corsairs ya nchini Japan.

VIDEO: Kocha wa Simba SC ‘Uchebe’ Yaliyopita yamepita jamani

Soma na hizi

Tupia Comments