AyoTV

Wastue wana Ndondo Cup 2018 imerudi

on

Kamati ya mashindano ya Sports Extra Ndondo Cup 2018 chini ya mwenyekiti wake Shaffih Dauda leo March 9 2018 imetangaza kuzindua rasmi michuano hiyo kwa mwaka 2018, kamati ya Ndondo leo imezindua michuano hiyo na kutangaza maboresho kadhaa ambayo hufaniyika kila mwaka.

Michuano hiyo imenzinduliwa leo na kuja na baraka baada ya moja kati ya kampuni kubwa za vifaa vya michezo duniani, Macron kutangaza kuwa wameingia kuwa wadhamini wa Ndondo na watagawa vifaa kwa timu zote 32 zitakazoshiriki na jumla ya mipira 1000, jezi za waamuzi na jezi za mashabiki wa michuano hiyo ikiwa ni moja kati ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa mwaka huu.

Usajili wa timu shiriki za Ndondo Cup watatakiwa kulipia Tsh 300,000/= kwa kila timu na zitalipiwa kupitia account ya chama cha mpira Dar es Salaam DRFA, kampuni ya ubashiri ya mCheza na Beko na wao wamekubali kuingia kama wadhamini wa michuano hiyo lakini kubwa pia mwaka huu waandaaji wataanzisha Ndondo Cup Academy kwa ajili ya kuinua vipaji.

RATIBA YA MATUKIO YA SPORTS XTRA NDONDO CUP 2018

NO. TAREHE TUKIO ENEO
1. 9 March 2018 Press conference-Ufunguzi msimu

Kuanza kwa Usajili wa timu shiriki

Dar es salaam (escape one)

Ruvuma

Mwanza

2. 6 April – 6 May 2018 Hatua ya awali Dar es Salaam

Viwanja….

v Kinesi

v Mabatini tandika

v Benjamini mkapa

v Ukombozi

v Airwing ukonga

v Bandari

3. 25 May 2018 v Hafla ya upangaji makundi 32 bora.

v Semina kwa viongozi wa timu shiriki.

v Ugawaji wa vifaa kwa timu na waamuzi.

 

Dar es Salaam (escape 1)
4. 1 June – 22 Julai 2018 Hatua ya 32 bora….

v 1 – 24 june-Michezo ya makundi.

v 25 june-Droo ya 16 bora mtoano.

v 27 june -4 julai-Michezo ya 16 bora mtoano.

v 2 julai-Droo ya robo fainal.

v 6 – 9 julai – Michezo ya robo fainal.

v 9 julai- Droo ya nusu fainal.

v 14 – 15 julai-Michezo ya nusu fainal.

v 20 julai – Mchezo wa mshindi wa tatu.

v 22 julai – Fainali Ndondo Cup

Dar es Salaam

Viwanja….

v Bandari

v kinesi

5. 28 Julai 2018 Usiku wa tuzo za Ndondo Cup Dar es Salaam (clouds media)
 
6. 18 Aug -22 Sept 2018 Ndondo Cup mkoani Ruvuma Songea

Mbinga

7. 5 Oct – 10 Nov 2018 Ndondo Cup Mkoani Mwanza Mwanza
8. 15 – 22 Dec 2018 Ndondo Super Cup Dar es salaam

UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu baada ya sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry

Soma na hizi

Tupia Comments