Kiungo wa kimataifa wa Kenya anayeichezea Totteham Hotspurs ya England Victor Wanyama kwa sasa vijana wengi wa Afrika Mashariki wanamtazama kama Role Model wao kutokana na hatua ya mafanikio aliyopiga katika soka kwa kuwa mchezaji pekee wa Afrika Mashariki anayecheza EPL.
Inawezekana hufahamu magumu aliyowahi kupitia Wanyama na umekuwa ukisikia tu stori za kulipwa kwake pound 70,000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 150 kwa wiki lakini Wanyama amewahi kupitia changamoto ya kurudishwa nyumbani kisa ada na vitu kama hivyo.
Wanyama katika kikosi cha Tottenham ni mchezaji wa 11 kwa wanaolipwa mishahara mikubwa akilingana na Erick Lamela, Erick Dier, Davinson Sanchez, Serge Aurier wakiongozwa na golikipa wao Hugo Lloris anayelipwa mshahara wa pound 120000 kwa wiki.
Hivi ndio Simba walivyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Al Masry