Mix

The Lost Hearts mkasa wa kimapenzi unaowahusisha marafiki wawili

on

Hivi utafanya nini endapo rafiki yako mpendwa kakuchukulia mpenzi wako? Hiki ni kionjo tu ndani ya Tamthilia ya The Lost Hearts, ambapo waigizaji nguli na wahusika wakuu wa tamthilia hii Tessa na Magra ambao ni marafiki wakaribu sana wanakuja kua maadau kwa sababu tu ya usaliti.

Wawili hao mmoja wao anamsaliti mwenzake kwa kutembea na mpenzi wa mwenzie, hii tamthilia itatuonyesha namna inavyotesa kwa kufahamu rafiki yako mpendwa kukuchukulia mpenzi wako.

Tessa ambaye ni mbunifu wa mitindo na Marga ambaye ni malkia wa urembo na model, ni marafiki wa karibu wanaoshirikiana kutimiza ndoto zao licha ya ugumu wa maisha yao, dhamana yao inapimwa wakati Caloy anaingia katika maisha yao. Caloy ana uhusiano wa kihistoria na Marga.

Lakini anapendelea kuweka mahusiano ya siri. Kisha Caloy akakutana na Tessa na wakapendana, ambapo wakasababisha Marga abadilishe uamuzi wa kumrudisha kwake. Wakati huo huo, mahusiano ya Caloy na Tessa yanajaribiwa wakati Jaime, bosi wa Tessa na mjane wa marehemu ya Tessa, anapoanza kumpendelea.

Hii inaitwa The Lost Hearts usikose Jumapili hii ni tamthiliya ya kuvutia, itaanza kurushwa siku ya Jumapili 27 October kwenye chaneli ya ST Novela Eplus saa 3:45 Usiku. Tamthilia hii itakuja baada ya Tamthilia ya Blood Sisters kuisha.

VIDEO:PYRAMIDS FC IMEWASILI JIJINI MWANZA NA NDEGE YA KISASA

Soma na hizi

Tupia Comments