Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ameamua kwenda Saudi Arabia Macca kwa ajili ya ibada ya umrah.
Mbwana Samatta kupitia ukurasa wake wa instagram akiwa na mchezaji mwenzake raia wa Gambia ambao wanacheza wote katika club ya KRC Genk Omar Colley wamepost picha wakiwa pamoja katika ibada ya umrah.
Kitendo hicho Samatta na Colley kwenda hija anaungana na mastaa wengine wa soka dunia ambao pia wamewahi kwenda Macca kufanya ibada ya umrah kama Mesut Ozil wa Arsenal na Paul Pogba wa Man United ambao nao ni waumini wa dini ya kiislam.
Yametimia maneno ya mchambuzi mkongwe Dr Leaky kuhusu Champions League