Leo August 31 2018 Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wamewasilisha ripoti ya nusu mwaka kwa haki za binadamu ambapo Mtafiti wa ripoti hiyo Fundikira Wazambi amesema kuwa rushwa ya ngono makazini na vyuoni bado ni changamoto kubwa ikiwemo upande wa wanahabari wa kike.
‘Kuna rushwa ya ngono maeneo ya kazi kituo kimeona bado ni tatizo kubwa maeneo ya kazi, wanawake ambao wanaenda kutafuta kazi, mabinti wanaombwa sana rushwa ya ngono ili waweze kupewa kazi au hata kupandishwa cheo, na hii pia imeonekana pia ni tatizo kubwa miongoni mwa wanawake ambao wako kwenye tasnia ya habari’ Fundikira Wazambi
BAJAJI ya kwanza kutengenezwa na Mtanzania “imekosa kibali’