Habari za Mastaa

Album ya Chris Brown mbioni kushika namba 1 chart za Billboard

on

Kwa mujibu wa mtandao wa Rap Up umeweka wazi kuwa mauzo ya Album ya Chris Brown ‘Indigo’ yanatarajiwa kutoka 110,000 na kufikia 135,000 katika wiki yake ya kwanza, huku ikiripotiwa kuwa nakala 50,000 zikiwa ni mauzo halisi .

Album hiyo ambayo iliachiwa rasmi Juni 28,2019 imeelezwa kuwa itakuwa itakuwa namba 1 kwenye chart za album bora za Billboard 200 kwa wiki ijayo kutokana na ukubwa wa mauzo uliofikia baada tu ya kuachiwa siku chache kwenye mitandao ya kupakua Album hiyo.

Inatajwa kuwa album hiyo ya tisa kutoka kwa Chris Brown yenye jumla ya ngoma 32, itakuwa ni album yake ya tatu kufikia namba 1 kwenye chati za Billboard 200 ikifuata na Album yake ya F.A.M.E ya mwaka 2011 na Fortune ya mwaka 2012.

VIDEO: JAMAA ANAYEFANANA NA JUX ARUSHA “NIKIENDA SEHEMU NAKAA VIP”

Soma na hizi

Tupia Comments