Michezo

DONE DEAL: Higuan ametua Stamford Bridge

on

Staa wa kimataifa wa Argentina Gonzalo Higuan leo mapema amewasili jijini London England kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake wa kutoka AC Milan kwenda Chelsea, Higuan amewasili mapema kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya katika kikosi hicho.

Higuan alikuwa kwa mkopo AC Milan akitokea Juventus ya Italia pia, Higuan anajiunga na Chelsea ikiwa ni siku chache zimepita toka Chelsea wameripotiwe kuruhusu Alvaro Morata kwenda Atletico Madrid ya Hispania kwa mkopo, hivyo Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri anaona ni chaguo sahihi kwake kumleta Higuan.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Maurizio Sarri aliwahi kumfundisha Gonzalo Higuan mwaka 2015-2016 akiichezea Napoli na baadae 2016 alihama timu hiyo na kujiunga na Juventus kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenda AC Milan, Higuan ambaye ni mali ya Juventus atacheza Chelsea kwa mkopo wa miezi sita tu hadi mwisho wa msimu.

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments