Michezo

Usishangae ukisikia Sanchez amejiunga na Man United

on

Taarifa zinazoripotiwa kwa sasa kuhusiana na staa wa kimataifa wa Chile anayecheza soka la kulipwa katika club ya Arsenal ya England Alex Sanchez, ameripotiwa kuwa yupo mbioni kujiunga na Man United katika kipindi hiki cha usajili cha dirisha dogo.

Sanchez pamoja na kuhusishwa kwa muda mrefu na tetesi za kujiunga na Man City leo Ijumaa ya January 12 2018 imeripotiwa na mitandao kadhaa Ulaya kuwa staa huyo amebadilisha mawazo na badala yake anajiandaa kufikia makubaliano binafsi na Man United ili kujiunga nao.

Alex Sanchez kama dili lake la kujiunga na Man United itatimia na kuihama Arsenal, atakuwa anaondoka Arsenal baada ya kudumu nayo kwa kipindi cha miaka mitatu na alijiunga nayo mwaka 2014 akitokea FC Barcelona ya Hispania alipodumu napo pia kwa miaka mitatu.

Alichokifanya Simon Msuva kwa Wakati Ujao Youth Academy

Soma na hizi

Tupia Comments