Baada ya headlines za kudaiwa Bongo Movie imekufa kutokana na uharamia wa kazi za sanaa, sasa hivi wasanii wa Bongo Movie wameamua kujikita zaidi katika kuziuza filamu zao katika TV stations kuliko kuuza tena katika mfumo wa DVD ambao umekumbwa na changamoto kubwa katika upande wa usambazaji.
Ili kurejesha ladha ya filamu za nyumbani maarufu kama Bongo Movie, ambayo kwa muda mrefu watazamaji wameikosa. Msimu huu wa Siku kuu StarTimes wataonyesha jumla ya filamu 25 katika kipindi cha mwezi mzima wa Disemb ikiwemo filamu ya Red Light ya Irene Uwoya itakayooneshwa Ijumaa hii.
Filamu hiyo inamuelezea kijana wa miaka 27 ambaye baba yake aliuwawa na rafiki yake huku mkewe akipona, kisa kikiwa ni pete ya utajiri. Mama na kijana wake wanaamua kuhama mji na kwenda kuishi sehemu nyingine ambako wanakutana na kijana anayewapatia habari kuhusu muuaji wa baba wa familia yao.
Hivyo wanasafiri kumtafuta muuaji huyo na mwishoni wanakuta akiwa amefariki hivyo wanaichukua pete ya utajiri ambayo ilichukuliwa baada ya mauaji ya baba yao, na kuwa matajiri tena, Filamu nyingine zitakazoonekana wikendi hii ni Agent Bavo na Akili Kichwania ambayo imemshirikisha mshekeshaji Haji Salum maarufu kama Mboto.
SHILOLE KAFUNGUKA “Wolper aolewe sasa, nimeamia kwangu madili mengi”