Michezo

Pogba na Rashford wamvulia kofia Ronaldo kabla ya game

on

Usiku wa November 7 2018 Man United watakuwa tena uwanjani mjini Turin kucheza game yao ya nne ya Kundi H dhidi ya wenyeji wao Juventus, ikiwa ni wiki mbili zimepita toka wapoteze katika mchezo wa kwanza kwa kufungwa kwa goli 1-0 lililofungwa na Paulo Dybala dakika ya 17 katika uwanja wa Old Trafford.

Kuelekea mchezo huo wachezaji wa Man United wameonekana kumsifia na kuukubali uwezo wa staa wa Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo na kuelezea uwezo wake mbele waandishi wa habari, Pogba anukuliwa “Ni kitu kikubwa sana kwa Juventus kuwa na mchezaji anayeza kufunga kirahisi kama anakunywa maji”

“Kwangu hakuna mchezaji anayenivutia katika soka kama Ronaldo, hakuna wachezaji wanaofanya hivyo wakiwa na umri wake, wengi wamekuwa  na kiwango cha juu na kushuka baadae lakini alivyoanza kila siku anakuwa juu juu”>>>Marcus Rashford

Juventus wanaongoza Kundi H lenye timu za Man United, Valencia na Young Boys na kama wakishinda leo mchezo wao watakuwa wamefuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments