HekaHeka

Hekaheka ya Novemba 27 nimekurekodia iko hapa, inatoka Ilala, Dar.

on

88.5Msichana mmoja anayeitwa Aisha ambaye imesemekana amekuwa akieneza maneno ya uongo kuhusiana na watu mbalimbali, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kusutwa na wanawake kutokana na vitendo hivyo.

Siku aliyobainika wanawake hao wamesema Aisha alimpigia simu mwenzake mmoja kwamba kuna kundi la wanawake wapo saluni wanamsema na baada ya kufika wakabaini kuwa msichana huyo ndiye aliyesema.

Wanawake waliokuwa katika tukio hilo wamesema kutokana na tabia hiyo alishindwa kuishi na mama yake na kupokelewa na mama yake wa hiari ambaye naye amesema kuwa kutokana na tabia za msichana huyo amelazimika kumfukuza.

Wakati wanawake hao wakisema namna ambavyo amekuwa akieneza uongo huo, Aisha hakuwa na neno lolote kujitetea kama ni kweli au hapana.

Unaweza kubonyeza play hapa kuisikiliza Hekaheka hiyo ambayo leo ni sehemu yake ya kwanza na sehemu ya pili itakuwa siku ya kesho.

Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments