Mix

Habari kubwa zilizoruka kwenye Televisheni za Tanzania usiku July 3, 2017

on

July 3, 2017 kupitia Televisheni za Tanzania zimeruka habari kadhaa za siasa, uchumi, jamii na utamaduni na kama ulikosa taarifa hizo kupitia Televisheni nimekuwekea hapa story kubwa mbili miongoni mwa habari nyingi zilizosomwa kupitia Channel 10 na Clouds TV.

Habari ya Clouds TV – Ziara ya siku mbili ya Rais Magufuli Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, leo July 3, 2017 amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambako alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa.

Akiwa katika ziara hiyo Rais Magufuli atazindua mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira Wilaya ya Sengerema July 4, 2017.

Habari ya Chanel 10 – Wananchi hawana elimu ya kutosha kuhusu Fedha za Mfuko wa Jimbo

Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ameshauri wananchi waelimishwe kuhusu umuhimu wa fedha za Mfuko wa Jimbo hatua itayowawezesha kusimamia miradi ya maendeleo inayosimamiwa na mfuko huo pamoja na kuepusha baadhi ya viongozi kufanya ubadhilifu wa fedha hizo.

Mmoja wa wananchi hao Boniface Matayo amesema awali hawakufahamu kama fedha za Mfuko wa Jimbo zinaweza kuwasaidia kutatua changamoto za kimaendeleo huku wengine wakidai kuwa fedha hizo hutolewa na Mbunge binafsi.

>>>“Hii habari ya kuambiwa hizi fedha ndio Mfuko wa Jimbo maana hii ndiyo mara ya kwanza. Zamani ilikuwa labda Mbunge akija kusaidia kutengeneza bomba katoa Elfu Ishirini anasema kama kasaidia kujitolea mwenyewe.” – Boniface Matayo (Mwananchi)

Msanii wa Bongo Movie afungua kanisa lake DSM 

Soma na hizi

Tupia Comments