Habari za Mastaa

Inadaiwa Drake kaamua kununua ndege na kuiita ‘Air Drake” (+video)

on

Rapper Drake ameamua kuonyesha ndege binafsi (Private Jet) kupitia ukurasa wake wa instagram inayosemekana kuwa ameinunua ikiwa bado haijawekwa wazi thamani ya ndege hiyo ambayo imepewa jina la ‘Air Drake’.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Drake aliandika “Hakika ,hakuna kitu kilichokuwa sawa”. Rapper huyo anatajwa kuwa miongoni mwa mastaa wenye pesa nyingi Marekani ambapo inaelezwa kuwa aliwahi kununua nyumba ya jirani yake kwa thamani ya Tsh Shilingi Bilioni 6 za Kitanzania baada ya jirani huyo kutoa malalamiko kuwa Drake hupiga sana kelele.

Rapper huyo kutokea Canada inaelezwa kuwa ana nyumba tatu tayari , ambapo moja ipo mjini Los Angeles Marekani iliyomgharimu zaidi ya Billioni 10 za Kitanzania nyumba mbili zipo katika makazi ya kifahari ya Hidden Hills ikiwa mjengo wa kwanza alinunua mwaka 2012 na mwaka 2015 alinunua nyumba nyingine iliyogharimu zaidi ya Billioni 4 za Kitanzania.

VIDEO: WOLPER AFIKA HADI MACHAME KUMZIKA MENGI AFUNGUKA ALIVYOGUSWA NA MSIBA HUO

Soma na hizi

Tupia Comments