Habari za Mastaa

Jay Z aamua kuajiri Mwanasheria kumsaidia 21 Savage

on

Baada ya sakata la Rapper 21 Savage kukamatwa siku kadhaa zilizopita na maafisa wa Uhamiaji Marekani inaripotiwa kuwa rapper Jay Z ameingilia kati sakata hilo na kumuajiri mmoja wa Wanasheria ‘Alex Spiro’ kusimamia kesi hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Pitchfork umeripoti kuwa Jay Z amesema kuwa 21 Savage anahitaji kuwa na nafasi ya kulea watoto wake na hatoaacha kumsiadia Rapper huyo mpaka atakapoachiwa huru.

“Kukamatwa kwa 21 Savage ni kumyang’anya Visa yake ambayo imesisitishwa kwa miaka minne na kutokana na yeye kuwa mwanamuziki aliyefanikiwa anahitaji kuungana na watoto wake haraka iwezekananvyo” >>>Jay Z 

Kwa mujibu wa maaafisa wa Uhamiaji nchini Marekani wameripoti kuwa 21 Savage alizaliwa nchini Uingereza na kuingia nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 7 baadae aliondoka na kurudi nchini humo 2005 na visa yake kuisha 2006.

LIVE: Ziara ya Wasanii Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa DSM kuitazama reli ya kisasa

Soma na hizi

Tupia Comments