Habari za Mastaa

Dogo Janja kuhusu Uwoya ‘Namiss kumpiga makofi, moment ni nyingi”

on

Mume wa zamani wa Irene Uwoya, Dogo Janja ameongelea vitu anavyovikosa kwa Irene baada ya wawili hao kutengana na kusema kuwa ana-miss kumpiga makofi na amefunguka na kuweka wazi kuwa kuna vitu ambavyo wameshafanya pamoja.

Dogo Janja ameongelea ishu hiyo kupitia mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha XXL cha Clouds FM leo March 29,2019 baada ya kwenda kutambulisha ngoma yake mpya ya ‘Yente’ na aliongeza na kusema anafurahishwa na jinsi Irene Uwoya anavyopambana lakini anatamani kuona akifanya vitu tofauti na wengine.

“Namiss kumpiga makofi ,Kuna vitu vingi ambavyo tumefanya pamoja na Irene Uwoya moment ni nyingi kikubwa namiss kumpiga makofi, nafurahi kuona jinsi anavyopambana na toka zamani nilikuwa natamani kuona akifanya vitu vyake na kumtofautisha na watu wengine” >>>Dogo Janja

EXCLUSIVE: Kutana na Photographer anayeuza picha Tsh Milioni 8

Soma na hizi

Tupia Comments