Waziri Mkuu wa Israel Binyamin Netanyahu amesema Israel “itatoza gharama kubwa kutokana na uvamizi wowote dhidi yeo kwa upande wowote Katika taarifa yake ya kwa umma tangu kuuawa kwa kiongozi mkuu wa kisiasa wa Hamas, Ismail Haniyeh.
Watu wasiopungua 17 walijeruhiwa katika shambulio la ndege isiyo na rubani ya Hezbollah kaskazini mwa Israel siku ya Jumanne huku kukiwa na hofu ya kutokea vita kamili kati ya pande hizo mbili, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel.
Jeshi la Israel limesema ndege kadhaa zisizo na rubani zilirushwa kutoka Lebanon hadi kaskazini mwa Israel huku ndege moja isiyo na rubani ikinaswa na nyingine kuanguka katika mji wa Nahariya.
Kwingineko Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Jumanne alimtaka kiongozi mpya wa kisiasa wa Hamas Yahya Sinwar kukubaliana na usitishaji mapigano Gaza.
Jeshi la Israel na mamlaka zinamtuhumu Yahya Sinouar kuwa mmoja wa wahusika wakuu wa shambulio la Oktoba 7.
Dakika chache baada ya kutangazwa kwa uteuzi wake, safu ya makombora ilirushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel, tawi la kijeshila Hamas lilidai kufanya hivyo.
“Kuteuliwa kwa gaidi mkuu Yahya Sinouar mkuu wa Hamas, kuchukua nafasi ya Ismaïl Haniyeh, ni sababu ya ziada ya kumuangamiza haraka na kufuta kabisa kundi hili,” amejibu Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz , kwenye mtandao wa X.
Lakini Afisa wa Hamas amesema kuteuliwa kwake kunatuma “ujumbe mzito” kwa Israeli, miezi kumi baada ya kuanza kwa vita katika Ukanda wa Gaza, vilivyochochewa na shambulio ambalo halijawahi kutekelezwa na Hamas katika ardhi ya Israel mnamo tarehe 7 Oktoba.
Mshirika wa Hamas wa Lebanon Hezbollah alimpongeza Sinwar na kusema uteuzi huo unathibitisha “adui… ameshindwa kufikia malengo yake” kwa kuwaua viongozi na maafisa wa Hamas.