Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Arusha imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na Mawakili wa utetezi wanaomuwakilisha mshtakiwa wa pili Sylivester Nyegu katika kesi ya Unyang’anyi wa kutumia Silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.
Huku Shahidi wa nne wa upande wa utetezi akisema mashtaka yaliyopo ni ya uongo na yametengenezwa na majina yaliyopo kwenye mashtaka sio ya kwake