Hospital ya Kinondoni Iliyoko jijini Dar es Salaam kushirikiana na hospital ya HCG iliyoko Mumbai, India imetambulisha program yao ambayo wanatarajia kuifanya tarehe 13 na 14 mwezi huu wa kumi mwaka 2023.
Ambapo program hiyo inalengo la kuwasaidia wagonjwa wanaosumbuliwa na Saratani lakini pia wale ambao wanadalili za Saratani, Wagonjwa watakutanishwa na madaktari bingwa wa saratani kutoka India na kuweza kujipatia matibabu na ushauri kutoka kwa madaktari hao.
Akizungumza na waandishi wa habari mganga mfawidhi wa Hospital ya Kindoni Dkt. Charles Basil Kafaiya amesema “Sababu ya kuanzisha program hiyo kwa wagonjwa wa saratani, ni kwa sababu katika hospitali yetu tunapokea wagonjwa wengi ambao mara nyingi wako kwenye stage za juu zaidi za kansa”
Ambapo ameongeza kwa kusema kuwa program hiyo inawahusisha watanzania note ambapo wamewasogeza madaktari hao kutuka India hili kutoa msaada kwa wagonjwa wote wa saratani