Tiba Jumuishi (Medical Assisted Treatment-MAT) hutolewa kwa Waathirika wa dawa za kulevya ikihusisha ushauri nasaha, matibabu ya kurekebisha tabia pamoja na utoaji dawa aina ya Methadone, ambapo katika Kliniki iliyopo MNH Upanga jumla wa Wananchi 1,100 wenye uhitaji huo wanahudumiwa kwa siku.
Mipango hiyo imeelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi alipofanya ziara kijijini hapo ambapo alipokea taarifa ya kijiji hicho na kuzungumza na Wagonjwa na Watumishi.
Aidha Prof. Janabi aliridhishwa na namna kazi za uzalishaji zinavyofanyika kijijini hapo licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu.
“Tutashirikiana na sekta binafsi kuhakikisha tunafanya maboresho makubwa hapa ikiwemo kuzungushia uzio kwenye eneo lote na ekari 160, kujenga majengo mazuri, pamoja na kuanzisha makazi ya kisasa ya kusaidia waraibu wa dawa za kulevya (sober house) ambao watasaidiwa kitaalamu zaidi”