Katika kuunga mkono juhudi za Serikali Kwenye zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa Hospitali ya Rufaa Mtakatifu Francisco iliyopo Mji wa Ifakara Wilaya Kilombero Mkoani Morogoro imefanya zoezi la hamasa ya mbio fupi iliyoenda sambasamba na utoaji wa huduma za vipimo bure baadhi ya magonjwa pamoja na uchagiaji damu.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mtakatifu Fransisco Ifakara Solaus Method amesema lengo la hamasa hiyo ni kutambua mchago mkubwa wa Serikali ikiwemo kutoa fedha zaidi ya shilingi bilioni tatu ikiwemo zaidi ya million mia mbili Kila mwezi Ili kusaidia masuala mbalimbali ikiwemo ulipaji wa mishahara.
Amesema katika kuunga mkoni Serikali suala la uchaguzi kila wananchi wanapata fursa ya kushiriki kupiga kura Hospitali hiyo imetoa magari matano ambayo yatasaida Kubeba watu wenye uhitaji na wazee kutoka katika eneo moja hadi vituo vya katika vituo vya kupigia kura.
Naye mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Danstan Kyobya amesema hali ya usalama imeimarishwa katika maeneo yote hivyo wananchi wote waliojiandikisha wajitokeza Kwa wingi katoka vituo vya kupiga kura bila wasiwasi.
Amesema uchaguzi ni haki ya kila mtu hivyo kila aliyejiandikisha atumie nafasi hiyo kuchagua viongozi ambapo anaona wanafaa.
Kwa upande wake Abubakari Asenga Mbunge wa Jimbo la Kilombero amesema uchaguzi huu ni muhimu Sanaa Kwani viongozi wanaopatikana watasaidia kusukuma gurudumu la maendendeleo pamoja na usimamizi wa miradi Kwenye maeneo yao.
Nao baadhi ya wananchi walioshiriki zoezi hilo wamesema Wananchi wametakiwa kuacha kuchagua viongozi ambao wanatoa rushwa badala yake wanatakiwa kuchagua viongozi bora ambao wananadi sera zao bila kuonesha ubaguzi ikiwemo udini,ukabila au ubinafsi wa aina yeyote.
Betha John ni mmoja wa wakazi wa Mji wa Ifakara walioshiriki hamasa hizo ambapo amesema ili kupata viongozi bora ni lazima kushiriki katika kupiga kura .
Amesema viongozi wa vyama mbalimbali wameendelea kunadi sera zao hivyo wananchi hawatakiwa kutofanya makosa kwa kuchagua viongozi ambao wameonesha viashiria vya rushwa au ubaguzi wa aina yeyote.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika novemba 27 mwaka huu ambapo katika hamasa hiyo zaidi ya Watu mia tano wamejitokeza kushiriki.