Top Stories

Hospitali ya Rufaa ya Chato asilimia 90 imekamilika

on

Ujenzi wa Hospitali ya Kanda ya Chato umekamilika kwa asilimia 90 katika awamu ya kwanza ambayo makabidhiano ya miundo mbinu ya awamu hiyo ya kwanza yamepangwa kufanyika mapema mwezi Machi.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima wakati wa uwekaji jiwe la msingi la Hospitali hiyo ya Ukanda wa Chato lililowekwa na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi.

Dk Gwajima amesema hospitali hiyo ikikamilika itakuwa nauwezo wa kuhudumia wananchi milioni 14 kutoka Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora, Rukwa, Geita, na wilaya za Mikoa ya Mwanza na Shinyanga.

RAIS MAGUFULI ALIVYOMPOKEA RAIS WA MALAWI AIRPORT CHATO

Soma na hizi

Tupia Comments