Duniani

Hadi kufikia September 2013 hizi ni hoteli 10 zinazotajwa kuwa na muonekano usio wa kawaida (+Pichaz)

on

September 19 nakusogezea karibu yako muonekano usio wa kawaida wa hizi hotel zilizopo katika miji mbalimbali duniani, huenda uliwahi kutembelea nchi kadhaa lakini hukubahatika kuona uzuri na upekee wa majengo ya hizi hoteli. Hii ni list ya hoteli 10 zisizokuwa na muonekano wa kawaida, yaani ziko tofauti na majengo ambayo tumezoea kuyaona.

1- Grand Lisboa Hoteli

grand_lisboa_resort_macau

Grand Lisboa Hoteli hii ni hoteli ambayo ipo Macau China, jengo lake lina urefu wa mita 258, upekee wa jengo hili limejengwa katika muundo wa ua ambalo kwa juu linachanua.

2- Barin Ski Resort

barin_ski_resort

Barin Ski Resort hii ipo Iran muonekano wa jengo lake ni kama lina ukungu wa theluji mbele.

3- Ryugyong Hoteli

ryugyong_hotel

Ryugyong Hoteli ipo Korea Kaskazini ni jengo lenye muundo wa Pyramid lakini sifa yake nyingine ni kuwa limejengwa kwa muda mrefu toka mwaka 1987 ndio lilianza kujengwa ila hadi September 2013 bado ilikuwa inaripotiwa kuwa linaendelea kujengwa.

4- Axis Viana hoteli

hotel_axis_viana

Axis Viana hoteli ipo Ureno muundo wa jengo lake ni kama box au sanduku la kuwekea mafaili.

5- Inntel Hoteli

inntel_hotel (1)

Inntel Hoteli iliyopo Uholanzi hii imejengwa kwa muundo wa nyumba za asili ya kidachi yaani kijumba kimoja kimejengwa juu ya kingine.

6- Aviator Hoteli

aviator_hotel

Aviator Hoteli ipo Uingereza imeingia katika hii list kwa kuwa wameitaja kuwa na muonekano wa ndege.

7- Burj al Arab

burj_al_arab_2

Burj al Arab hii ipo Dubai mtu wangu imejengwa kwa muundo wa lile pazia ambalo linatumika kuongozea ngalawa ambazo zilitumiwa na waarabu kuja Afrika.

8- Taj Lake Palace

taj_lake_palace

Taj Lake Palace Hoteli ipo India mtu wangu upekee wake ni kuwa muonekano wake ni kama inaelea kati kati ya ziwa.

9- Hotel Unique

hotel_unique_3

Hotel Unique hii ipo Brazil imejengwa kwa muundo wa kipande cha tikiti maji.

10- Hotel Marqués de Riscal

marques_riscal_hotel

Hotel Marqués de Riscal mjengo wa hoteli hii ya Hispania, muonekano wake ni ngumu kulinganisha na kitu ila umepambwa kwa rangi flani hivi za kinywaji cha wine.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments