Top Stories

House boy ahukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kulawiti

on

Mahakama ya Wilaya ya Tarime imemuadhibu kifungo cha maisha Jela mfanyakazi wa nyumbani, Magige Thomas (21) baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kiume wa mwaka 1 na miezi 5.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Salum, alidai Magige alitenda unyama huo Agosti 5, 2019 mchana, wakati wazazi wa mtoto huyo wapokuwa kazini.

Upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi 4 na kuithibitishia Mahakama kuhusiana na kitendo hicho ikiwamo taarifa za Polisi (PF3), mganga na wazazi huku upande wa utetezi ukiwa bila shahidi.

Wataalamu wa Saikolojia wanasema ongezeko la matukio ya ukatili dhidi ya watoto nchini yanachagizwa na mambo mengi zikiwamo imani za kishirikina na jamii kutokuwa na hofu ya Mungu.

AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA “ALIMCHINJA MTOTO WAKE PORINI”

Soma na hizi

Tupia Comments