Habari za Mastaa

Picha 5 za utani uliosambazwa baada ya Solange kumpiga ‘shemeji’ Jay Z

on

Screen Shot 2014-05-13 at 10.58.04 AMBaada ya kuvuja kwa video ikionyesha jinsi rapper Jay Z akipigwa na shemeji yake (Solange) wakiwa kwenye lift huku Beyonce mwenyewe akiwa pembeni yao akishuhudia ugomvi bila kujihusisha wala kuzuia, uongozi wa hoteli ugomvi huo ulipotokea huko New York umesema unachunguza kujua video hiyo ilivuja vipi na kupeleka siri za wateja kwenye vyombo vya habari.

Kwenye ugomvi huu ambao Jay Z ameonekana kusifiwa na watu wengi kwa kuwa mkimya na bila kujibu mashambulizi pamoja na kupigwa mateke na kurushiwa vitu, tayari watundu wa mitandaoni wameanza yao kwa kutengeneza picha na maandishi vikimtania Jay Z pamoja na Solange.

Screen Shot 2014-05-13 at 10.57.08 AM

Screen Shot 2014-05-13 at 10.58.23 AMKutokana na ile single ya Jay Z iitwayo ’99 problems’ yaani matatizo 99… watu wamemtengenezea utani kwamba Solange ni tatizo la 100 la Jay Z.

Screen Shot 2014-05-13 at 10.58.40 AM

Screen Shot 2014-05-13 at 10.59.01 AMSehemu ya utani mwingine ni hii ya historia kwenye wikipedia ya Solange na kuifanya itoe maelezo kwamba Solange ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, kicker, streetfighter na tatizo la 100 la Jay Z.

Screen Shot 2014-05-13 at 10.59.36 AMScreen Shot 2014-05-13 at 12.06.56 PM
Ili niwe nakutumia stori kila zinaponifikia jiunge nami twitter kwa kubonyeza HAPA, facebook >> FB na instagram INSTA

Soma na hizi

Tupia Comments