Habari za Mastaa

Maneno ya kwanza ya Jacqueline kwa Mumewe Dkt. Reginald Mengi

on

Ikiwa tayari zimepita siku 27  tokea kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za IPP Dkt. Reginald Mengi kufariki mkewe ambaye ni Jacqueline Mengi amekuwa kimya kwenye mitandao ya kijami na leo ameandika ujumbe kwa mume wake ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa.

“Leo tungekuwa tuna kusheherekea wewe, kama nikifumba macho yangu naweza kuona namna unavyo tabasamu pale tunapokuimbia heri ya kuzaliwa. Hakuna neno la kuelezea ni kiasi gani Mimi na watoto tulivyokukumbuka, kuamka kila siku bila wewe. Heri ya kuzaliwa mpenzi wangu wa kweli, milele mioyoni mwetu.” ameandika Jacquline kupitia ukurasa wa Twitter.

Dkt Reginald Mengi ameacha jumla ya watoto wanne ambapo watoto wawili mapacha wa kiume alizaa na Jacquline Mengi na leo hii May 29,2019 angekuwa akitimiza miaka 75. Marehemu Reginald Mengi alifariki May 2,2019 akiwa Falme za Kiarabu Dubai kwa ajili ya matibabu.

VIDEO: “Ukitualika tunakuja tunafuturu tunapiga selfie tunasepa” Roma Mkatoliki

Soma na hizi

Tupia Comments