Nyumba/ Mijumba

PICHA 9: Kwa mnaopenda kujenga Nyumba nje ya mji….

on

Hakika kila mmoja anapenda kuishi sehemu nzuri…. na hii post ni kwa wale wenye pesa zao ambao wanapenda kujenga nyumba nje ya mji na katikati ya eneo lenye mvuto lililozingirwa na miti na mazingira mazuri.

Kwenye pitapita zangu nikakutana na hizi picha nikasema sio mbaya nizisogeze kwako labda unaweza kuchukua chochote hapa mfano garden yenyewe ambayo haina vitu vingi lakini imependezesha sana hii sehemu.

Jinsi walivyozi-set taa pia imenivutia na vilevile ni nyumba ya gorofa lakini sio gorofa tulizozoea kuziona sana, haijawa na urefu sana kwenda juu na haina rangirangi nyingi kwa nje…. hicho ni miongoni mwa vilivyonivutia, iko simple 

Moja ya vinavyonivutia kwenye nyumba ni nyumba kutokuwa na vitu vingi ndani yake na vichache visivyowaka/visivyong’ara kuchukua nafasi … hii sehemu imenivutia sana pia

Kama umevutiwa na hii nyumba kwenye chochote sio mbaya ukiniachia comment yako mtu wa nguvu…. na ninataka tu kukwambia kwamba kama upo Dar es salaam, ujenzi wa nyumba yako unaweza kuwa rahisi sababu GSM MALL ya Pugu Road.

DANUBE ya GSM MALL PUGU ROAD ina vitu vingi vya ujenzi wa kisasa kama tulivyoona hapo juu, wako wazi Jumapili mpaka Jumapili mpaka saa mbili usiku.

Soma na hizi

Tupia Comments