Habari za Mastaa

Gigy Money “Sistahili kulipwa Milioni 1, bora nicheze mdako na mwanangu”

on

Mwimbaji Gigy Money ameamua kuyatoa ya moyoni kuhusiana na mapromota na kusisitiza kuwa kwa sasa yeye sio mwanamuziki underground na hastahili kulipwa shillingi milioni moja kwa ajili ya kufanya tamasha sehemu fulani .

Gigy Money amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa anastahili kizuri zaidi kwani show yake ya mwisho alilipwa hela nzuri na inabidi watu wafahamu kuwa kwa sasa yeye ni mama na vitu vinatakiwa kufanywa kitaaluma zaidi.

“Kuna Watu Wengine mkoje Sijuii Kwani ukinitangazia nakataa Show yani ndio sitofanya Show Naomba niiliweke hili swala sawa mm ni msanii tena Sio underground Afu pia ni mama swala lakukataa Kufanyaa Show ni maslahi Wala Sio kuringa Tangu mme anza kufanya Show sasa ni miaka 5 adi ujauzito wangu wote nipo stejini kama mapromota hiyo tabia yenu yakujifanya aaah”

“Gigy money namuweza kweli mmeniweza sana pia kama Show za M1 nishafanya nchi nzima kama nakula Vizuri Nalala nina furaha sina ulazima wakusononeka kweli maisha ni Magumuu lakini nawapa taharifa Sina Management inayo nipa jeuri wala bwana Angu anihongi hivyo kama mnavyokaa kuongea nachoamini I deserve better my last Show was WASAFI FESTIVAL NA nmelipwa Vizuri.”

“Sasa kwann mnitese kukata viuno,kukesha,kuimba Kusafirii kuwafata mashabiki Na bado heshima mtu upewi nasemaje million moja labda collaborations Na Sio Show . Bora nicheze Na Mwananguu mdako Jina langu kubwa mpaka saivi Sina ata gari kwa ujinga wakufanya kazi kwakulalamika afu unakuta mtu anatajirika tu kupitia majina ya watu mm mnisamehe saivi najitambua”

“Sio Interview za Onlinee wala Show za kusaidiana mambo Ni professional sikuizi (Na Wewe mwanamke endelea kutangaza Gigy anakataa Show ivyo ivyo ntakupost nikuchambe hapahapa) unafikili ata nisipo fanya Show Yako kwamba sitofanya Show jifanye domo lako bwaku langu mm bwabwajaaa 😡 Caption haisuani Na picha”

AUDIO :ULIPITWA NA HILI LA MWIGIZAJI WEMA SEPETU KUHUSU MAMA YAKE MZAZI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA

 

Soma na hizi

Tupia Comments