Michezo

PICHA: Matokeo ya EPL na msimamo, Man City imetoa dozi ya wiki kwa Watford

on

Club ya Man City imezichukua headlines kufuatia ushindi wa kishindo wa Ligi Kuu ya nchini England dhidi ya Watford, Man City ambao ni Mabingwa watetezi licha ya Watford kuwa na historia ya kuwasumbua vigogo lakini wamekutana na kipigo cha msimu.

Man City akiwa nyumbani ameifunga Watford kwa idadi ya magoli 8-0, magoli ambayo ni mara chache yanafungwa katika EPL kwa mechi moja, hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Watford kwani ndani ya dakika 18 za kwanza tayari walikuwa wamefungwa magoli 5-0.

Magoli ya Man City yalifungwa na David Silva dakika ya 1, Sergio Aguero dakika ya 7 kwa penati, Riyad Mahrez dakika ya 12, Bernaldo Silva aliyefungwa hart trick  dakika ya 15, 48 na 60, Nicolaos Otamendi dakika ya 18 na  goli la mwisho la Man City likafungwa na Kelvin De Bruyne dakika ya 85 ya mchezo.

Ushindi huo unaiweka Man City nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya England wakiwa na point 13 nyuma ya Liverpool wanaoongoza wakiwa na point 15 huku wakizidiwa mchezo mmoja, Liverpool wakisubiri kucheza na Chelsea Jumapili ya Septemba 22 2019.

VIDEO: Moja kati ya magoli ya marehemu Jeba, hili liliwaumiza wana-Simba 2016

Soma na hizi

Tupia Comments