AyoTV

VIDEO: Kauli ya Kocha wa Taifa Stars na Bocco baada ya kutua Nairobi

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars leo imewasilini jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya Harambee Stars wa kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika 2020 zitakazofanyika nchini Cameroon, baada ya kuwasili AyoTV imeongea nahodha John Bocco na kaimu kocha mkuu Etienne Ndairagije.

“Hatukupata matokeo kama tulivyoyatarajia lakini tunaamini tuna morali nzuri tumekuja hapa kuweza kupambana katika huu mchezo ili tuweze kuvuka hii hatua, ukiangalia matokeo hata ya nyumbani yakikuwa ya bila kufungana wao pia wanahitaji kutufunga ili tuweze kutoka” >>> John Bocco 

Taifa Stars itacheza mchezo wake wa marudiano na Harambee Stars Jumapili ya August 4 2019, hiyo ni baada ya mchezo wao wa kwanza kumalizika kwa sare 0-0, Taifa Stars ili isonge mbele itahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kufungana magoli.

VIDEO: Kauli ya Kaseja baada ya kuichezea Taifa Stars baada ya miaka 6

Soma na hizi

Tupia Comments