AyoTV

Zawadi ya MO Dewji kwa wachezaji wa Simba SC baada ya Ubingwa 2018/19

on

Ushindi wa 2-0 wa Simba SC dhidi ya Singida United jana May 21 uliifanya club hiyo kutangazwa kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2018/2019 kwa mara ya pili mfululizo, Simba SC walitangazwa Mabingwa wakiwa na game mbili mkononi kutokana na kufikisha point 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote Ligi Kuu.

Kufuatia Ubingwa huo muwekezaji wao na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Mohammed Dewji ‘MO’ ametangaza kuwa atatoa zawadi ya boda boda kwa wachezaji wote kama zawadi kwa kufanikiwa kutetea Ubingwa huo wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa mara ya pili mfululizo.

Mapokezi ya Sevilla Tanzania waliokuja kukipiga na Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments