Michezo

Kauli ya RC Makonda kwa wachezaji wa Taifa Stars 1980 ambao hawakuwepo Ikulu

on

Jana March 25 2019 Rais Magufuli akiwapongeza na kuwazawadia viwanja wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa kusaidia timu hiyo kufuzu kucheza fainali za AFCON 2019 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39.

Rais Magufuli hakumsahau Peter Tino mchezaji ambaye aliifungia goli Taifa Stars na kufuzu kucheza fainali za AFCON 1980, kwa kumpa Tsh milioni 5 baada ya kumuita na kumuuliza anafanya shughuli gani kwa sasa na kusema kuwa hana kazi.

Katika kikosi cha wachezaji wa zamani wa Tanzania walioipeleka timu AFCON 1980 jana alikuwepo Peter Tino na Leodgar Tenga pekee, RC Paul Makonda ambaye ni mwenyekiti wa kuhamasisha Taifa Stars ishinde AFCON 2019, leo amewaambia wachezaji hao kwa wasiofika maombi yao yamepokelewa na anayafanyia kazi, hivyo wasubiri tu kwa kuendelea kuwa wavumilivu.

MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS

Soma na hizi

Tupia Comments