Michezo

Robert Marawa kafukuzwa kazi Super Sports kwa SMS

on

Mtangazaji mahiri kituo cha Super Sports cha Afrika Kusini Robert Marawa ametangaza kuwa amefukuzwa kazi katika kituo hicho, Marawa ameeleza kuwa amefukuzwa kazi kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yake ya mkononi.

Taarifa za kufukuzwa kwake amezitoa mwenyewe kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter na kueleza kuwa alitumiwa meseji fupi, taarifa za kufukuzwa kazi kwa mtangazaji huyo zimewashitua wengi huku wakihoji chanzo ni kitu gani kilichopelekea.

“Niwashukuru wote kwa sapoti mliyonipa wakati wote wa safari yangu ya utangazaji wa michezo Super Sport na wale wote niliokuwa nafanya nao kazi SuperSport, siku moja wote mtafahamu ukweli utagharimu maisha yangu lakini mtajua tu”>>> Robert Marawa

Meseji aliyotumiwa inadaiwa ilikuwa inasema “Usijiangaishe kuja kwenye kipindi” Marawa pia amewahi kufukuzwa kazi 2017 na kituoa cha SABC ila inadaiwa hiyo inawezekana ni kutokana na kauli zake alizozitoa kuhusiana na madai ya unyanyasaji wa kingono.

Mzee Muchacho na Fahad wambananisha Haji Manara avae jezi ya Yanga SC

Soma na hizi

Tupia Comments