Michezo

Bodi ya Ligi ya tegua kitendawili kuhusu Kagera Sugar na Stand United

on

Baada ya kuenea kwa sintofahamu mitandaoni kuwa kati ya Kagera Sugar na Stand United ni timu gani imeshuka daraja, hatimae bodi ya Ligi Kutumia mtendaji Mkuu wake Boniface Wambura imeweka mambo sawa na kutolewa ufafanuzi kuhusiana na  mkanganyiko huo.

Awali TFF kupitia account yao rasmi ya instagram waliandika kimakosa kuwa Kagera Sugar ndio imeshuka daraja na Stand United kubakia Ligi, ila kwa mujibu wa mahesabu ni kuwa Kagera wanabakia kucheza Play Off na Stand United rasmi wanaaga michuano hiyo.

“Umejitokeza mkanganyiko kuhusiana na msimamo wa mwisho wa Ligi ambao tuliutoa na ufafanuzi ni kwamba kulikuwa na makosa kwa watu wa data kuhusiana na mechi inazizuhusisha timu za Kagera Sugar na Stand United, hii ni mechi ambayo ilichezwa May 16 katika uwanja wa Kaitaba na matokeo kwa mujibu wa rekodi Kagera Sugar alifungwa 3-1 lakini watu wa data wakaingiza 3-0 ila zimefanyiwa marekebisho”

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments