Katika Ulimwengu wa sasa watu wengi hupendelea kupost picha mbalimbali zikiwepo za watoto wao kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni kwa sababu mbalimbali. Hata hivyo inashauriwa watu kuwa makini na aina ya picha wanazoamua kuzipost.
Zimetajwa aina 5 za picha za watoto ambazo hazitakiwi na si salama mtu kupost kwenye mitandao ya kijamii juu ya watoto wao.
1. Wakiwa na watoto wengine
Katika nchi nyingi duniani ni kosa la kisheria kuweka hadharani picha ya mtoto popote hususani kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao hiyo ya kijamii pasipo ridhaa ya wazazi wake. Hivyo inashauriwa watu kutofanya kosa hili kwani hatua zinaweza kuchukuliwa dhidi yao.
2. Shule wanazosoma
Kwa sababu za kiusalama wazazi wanashauriwa kutoweka wazi kwenye mitandao ya kijamii shule ambazo watoto wao wanasoma. Watu wengi hupenda kuweka picha za watoto wao kwenye matukio kama siku yao ya kwanza kwenda shule, sherehe mbalimbali na mengineyo suala ambalo linasemwa kuwa baya na hatari.
3. Wakiwa zinazoonesha miili yao
Kuna wazazi pia hupendelea kupost picha za watoto wao ambazo zinaonesha miili yao kwa nyakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na wakati wa kuoga au kuvalishwa nguo, wakiwa beach au wakati wowote, suala hili limetajwa pia kuwa baya.
4. Kuelezea taarifa zao muhimu
Wazazi ambao hupost picha za watoto wao na kuandikia maelezo juu ya taarifa muhimu za maisha yao kama majina yao yote, vitu wanavyopenda kufanya kama kula, zawadi, maeneo ya kwenda na mengine ni tabia inayoelezwa kuwa ni hatarishi kwa usalama wa watoto hao.
5. Picha zitakazowaaibisha au kuweka wazi usiri wa aina fulani
Hili pia ni suala muhimu lililotajwa ambapo wazazi wameshauriwa kuacha kupost picha za watoto wao wakiwa wagonjwa, au wanapata matibabu (wamelazwa hospitali n.k), wamejisaidia na matukio mengine mengi ambayo kama watoto hao wataombwa ruhusa ya kuyapost hawatakubali.
ULIPITWA? Matano yaliyoibuka katika kesi ya Manji Mahakamani…TAZAMA HAPA!