Top Stories

UTAFITI: Watoto wa kwanza kuzaliwa huwa na akili zaidi kuliko wadogo zao

on

Utafiti uliofanywa unaonesha kuwa watoto wa kwanza kuzaliwa katika familia huwa na akili sana ukilinganisha na watoto wanaofuatia kuzaliwa.

Wataalamu wa Uchumi kutoka University of Edinburgh baada ya kuwa katika mjadala kwa miaka mingi wamehitimisha kuwa watoto wa kwanza kuzaliwa wanakuwa na kiwango cha juu cha IQ ukilinganisha na watoto wanaowafuata.

Watafiti wanasema majibu ya utafiti wao unaweza kuelezewa kwamba watoto wa kwanza kuzaliwa hupata mapenzi makubwa na support kubwa katika kuendeleza akili kutoka kwa wazazi wao katika kipindi cha miaka ya mwanzo. 

Matokeo ya utafiti huo yaliyochapishwa kwenye Journal of Human Resources, unaweza pia kuelezea kinachoitwa athari za kuzaliwa pale ambapo ndugu wakubwa katika familia hufurahia mshahara mzuri na elimu bora katika maisha yao ya baadaye, kwa mujibu wa Watafiti.

Pia wameeleza kuwa wazazi wengi hubadilika tabia pindi wanapopata watoto wengine ikiwa ni pamoja na kuwa na muda mchache kwa ajili yao hususani kwenye kucheza nao au kuwafundisha vitu mbalimbali.

Uliikosa hii?Kilichofanya RC Kagera kumuweka ndani Afisa kwa saa 48 

Soma na hizi

Tupia Comments