Top Stories

Rais Magufuli kaitolea majibu changamoto iliyompigisha magoti Mbunge

on

Siku chache zilizopita Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa alilazimika kupiga magoti kumuomba Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne kufikisha kilio cha maji cha wakazi wa Rwakajunju kwa Rais Magufuli.

Kupitia ziara ya Rais Magufuli wilayani Karagwe, Kagera, Mbunge huyo ameendelea kuwasilisha kilio chake kwa Rais akisema changamoto hiyo imekuwepo tangu utawala wa Rais Mkapa.

Akitolea majibu changamoto hiyo Rais Magufuli amesema kuwa anatambua uwepo wa changamoto kubwa ya maji katika Wilaya ya Karagwe ambapo amesema, ili kuhakikisha changamoto hiyo inaisha zimetengwa Tsh Bilioni 70 kwa ajili ya maji wilayani humo.

RAIS MAGUFULI: Alivyowataja wanaosema wanaidai Serikali MABILIONI

Soma na hizi

Tupia Comments