Habari za Mastaa

Cassper Nyovest akatishwa tamaa na muziki wa Afrika Kusini kutofika mbali

on

Rapper kutokea Afrika Kusini Cassper Nyovest amefunguka kuhusu game yao ya muziki kutofika mbali na kusema kuwa wasanii wengi hawapendi kufanya ushirikiano kwenye kazi na hupenda kupata mafanikio wao kwa wao na kwenye hilo ameshakata tamaa tayari .

Kauli za mkali huyo zimetoka baada ya shabiki mmoja kupitia mtandao wa twitter kuandika mawazo yake juu ya muziki wa Nigeria kwa jinsi unavyokuzwa na wasanii kama Wizkid, Davido baada ya Wizkid  kutumbuiza kwenye tamasha The Ends Festival na Davido alitumbuiza kwenye tamasha la Hot 97 Summer Jam Marekani.

“Muziki wa Nigeria bado upo mbele yetu sana, Wizkid anaongoza orodha ya watumbuizaji kwenye tamasha la The Ends Festival wikendi hiyo hiyo ambayo Davido anakichapa kwenye Summer Jam.” aliandika shabiki huyo kupitia twitter 

“Ujinga mwingi unaendekezwa Afrika Kusini ili kukua , watu hata hawataki kushirikiana kwenye nyimbo. Watu Wanataka kututhibitishia jinsi gani wanaweza kufanikiwa peke yao hatuwezi kufika, itakuwa ni kwa msanii mmoja mmoja na sio kwa wote. Nimekata tamaa.” >>>Cassper Nyovest

VIDEO: KUMEKUCHA MISS ILALA, MASHARTI YAMETOLEWA “ATAPATA MILIONI MOJA”

Soma na hizi

Tupia Comments