AyoTV

Yanga wametimia angalia walivyoimaliza KVZ FT 1-0

on

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Dar es Salaam Young Africans January 3 2019 ilicheza game yake ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya KVZ, Yanga ambao walileta wachezaji wa team B kwa kiasi kikubwa katika michuano hii walionesha uwezo.

Pamoja na mashabiki wengi kutarajia kuwa Yanga itafungwa katika mchezo huo kutokana na kuleta wachezaji wa team B, vijana hao wamedhihirisha kuwa Yanga wametimia kila idara hadi kikosi chao cha team B kinaweza kupata matokeo katika game muhimu.

Yanga walifanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Shabani Mohamed, hivyo Yanga sasa wanaongoza Kundi lako kwa kuwa na point tatu ila wana kazi ya kucheza dhidi ya Azam FC game ijayo January 3 2019 katika uwanja wa Amaan, kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya KVZ kilikuwa na Deusi Kaseke nahodha, Juma Makapu na Haji Mwinyi ndio wachezaji wa kikosi cha kwanza.

Kocha wa Simba baada ya kuwasili Zanzibar”Sio njia bora ya kuandaa timu”

Soma na hizi

Tupia Comments